NJIA ZA KUFAULU USAILI WA SEKRETARIETI YA AJIRA



NJIA ZA KUFAULU USAILI WA SEKRETARIETI YA AJIRA

Usaili wa Sekretarieti ya Ajira una namna tatu:

  1. Usaili wa Mchujo (Written Interview)
  2. Usaili wa Vitendo (Practical Interview) kwa baadhi ya kozi
  3. Usaili wa Mahojiano (Oral Interview)

1. USAILI WA MCHUJO (WRITTEN INTERVIEW)

Huu usaili hufanyika kwa watu wote waliokidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili. Kama jina linavyoeleza, usaili wa mchujo maana yake ni hatua ya kupunguza idadi ya waombaji ili kubaki na wachache. Maswali hayapo specific, hivyo inakulazimu kusoma kila kitu kinachohusiana na fani yako.

Mtu atauliza: Nitasomaje vitu vyote kwa wiki mbili? Inawezekana kusoma kwa wiki mbili vitu vingi kwa kufanya hivi:

  1. Tayari una basic knowledge kuhusu fani yako – hiyo itakusaidia.
  2. Angalia taasisi unayotaka kufanyia kazi au uliyotumwa kufanya usaili inajihusisha na nini.
  3. Chukua past papers zako za chuo kipindi unasoma – zipitie.
  4. Tafuta maswali ya walio wahi kufanya usaili Sekretarieti ya Ajira – hata kama siyo fani yako – ili ujue format.
  5. Soma job description ya tangazo la kazi na upitie kila kilichoandikwa. Ukiweza, chukua hiyo job description, muombe ChatGPT au mtu yeyote ayageuze kuwa maswali ya multiple choice au ya interview.

FORMAT YA USAILI WA MCHUJO (MARA NYINGI):

  1. Maswali ni ya aina ya Multiple Choice
  2. Idadi huwa kati ya 40 – 50
  3. Muda ni dakika 40 – 45
  4. Lugha ni Kiingereza
  5. Unaweza kufanya kwa kuandika kwa mkono au online (Amplitude Test) – yote ni sawa tu.

2. USAILI WA VITENDO (PRACTICAL)

Kwa baadhi ya kozi, mara chache hufanyika usaili wa vitendo. Mfano: kada ya afya au madereva. Hapa jiandae na vitu ambavyo hufanyika kazini kila siku na pia sheria zinazohusu taaluma yako.

  • Soma vitu vyepesi na vya msingi.
  • Hakikisha umefanya utafiti kuhusu taasisi hiyo – unajua vifaa au huduma wanazotoa.
  • Mfano: Kama unajua taasisi haina mashine ya GeneXpert kwa ajili ya TB, huna haja ya kuisoma.
  • Fahamu taasisi inajihusisha na nini.

Kumbuka: Katika hatua hii mmepunguzwa sana. Kwa kila nafasi moja, mnaweza kuwa watu 9 – au kutegemea na taasisi husika.


3. USAILI WA KUANDIKA AU ORAL INTERVIEW

Hii ni stage muhimu sana na inafaa ujipongeze. Kwa sababu zifuatazo:

  1. Upo hamsini kwa hamsini kupata kazi
  2. Ukifaulu kuanzia alama 50 unabakia kwenye database ndani ya mwaka mmoja – zikitokea nafasi unaitwa kazini tu
  3. Maswali unayoenda kufanya unayajua au yanajulikana

FORMAT YA USAILI

  1. Maswali ni 7
  2. Lugha ni Kiingereza
  3. Panel mara nyingi ni 7
  4. Muda ni dakika 15
  5. Swali la Tell me about yourself lipo – hata likibadilika uulizaji

TECHNIQUE

  1. Soma tangazo vizuri la kazi na kila job description ifanye kuwa swali na ulifanyie kazi. Kwani asilimia 80 ya usaili wa mahojiano wanatoa kwenye job description kwenye tangazo la kazi.
  2. Jiandae jinsi ya kujibu swali TELL ME ABOUT YOURSELF – nenda AjiraCoach Platform, utapata majibu namna ya kulijibu. Hili swali ndilo litakalokufanya upate kazi au ukose. Unaweza kuwa umejibu maswali yote lakini ukafeli hili, ukakosa kazi. Kwa hiyo hakikisha unalijibu vizuri sana hili swali. Ukifanikiwa kujibu vizuri hili – hata ukikosea mengine unaweza kufaulu.
  3. Jibu maswali kwa sauti inayo sikika vizuri
  4. Wasalimie hata kama umewazidi kiumri
  5. Usikae kwenye kiti mpaka wakuruhusu kukaa – hata kama umeona kiti
  6. Vaa vizuri na nyoa in proper way – yaani hakikisha huwaboi au kuwaudhi wasaili
  7. Mara nyingi usaili wa mahojiano utategemea na msaili na wewe mwenyewe – kwani huruma inaweza kuwepo


Post a Comment

0 Comments

Comments